MyElimu
Uandishi Wa Barua - Printable Version

+- MyElimu (https://myelimu.com)
+-- Forum: GENERAL STUDENTS DISCUSSIONS (https://myelimu.com/forum-general-students-discussions)
+--- Forum: KISWAHILI (https://myelimu.com/forum-kiswahili)
+--- Thread: Uandishi Wa Barua (/thread-uandishi-wa-barua)Uandishi Wa Barua - MyElimu - 10-19-2017

UANDISHI WA BARUA
Barua ni karatasi yenye ujumbe ulio katika maandishi. Au ni njia ya mawasiliano inayotumia maandishi kufikisha ujumbe, uandisha wa barua ni kitendo cha kuandika barua yenye ujumbe husika na kupeleka mahali panapohusika .
Kuna aina nyingi za barua, zikiwemo aina mbili rasmi za barua ambazo ni
 1. Barua za Kirafiki
 2. Barua za Kikazi
Barua za Kirafiki
Ni barua zinazoandikwa na watu au mtu kwa lengo la kupashana habari, kujuliana hali, kuonyana na kuomba kushukuru. Mara nyingi barua hizi huandikwa kwa ndugu, rafiki au watu wenye mahusiano mbalimbali katika jamii husika.

TARATIBU/MUUNDO WA UANDISHI WA BARUA YA KIRAFIKI
 1. Anuani ya mwandishi
Huandikwa juu ya karatasi upande wa kulia katika umbo la mshazari. Anuani ya mwandishi humsaidia aliyepelekewa barua kurudisha majibu ya barua.
 Mfano;
Shule ya sekondari Arusha
                             S.L.P 4051
                                 Arusha
 1. Tarehe
Chini ya anuani ya mwandishi tarehe huandikwa ili kumjulisha mpelekewa barua siku iliyoandikwa.                                                                                                                         
Mfano;
28/08/2026
 1. Mwanzo wa barua
Huandikwa mara baada ya tarehe na hukaa upande wa kushoto.                                                       
Mfano;
 Mpendwa Bushiri
 1. Kiini cha barua
Huanza na utangulizi ambapo hutolewa salam.                                                                                           
Mfano;
Habari za siku nyingi au salamu nyingi zikufikie na baada ya hapo ndipo   kiini cha barua huelezewa kwa kufafanua lengo au dhumuni la barua.
 1. Mwisho wa barua
Ni sehemu ya maaagano na huandikwa kwa maneno machache.                                                          
Mfano;
                    Wako rafiki
                    Wako kipenzi
 1. Jina la mwandishi
Humjulisha aliyepelekewa barua kujua ilikotoka.                                                                        
Mfano;
                    Abdallah Jabil
                    Ikram Saleh
 
 
MUUNDO WA BARUA YA KIRAFIKI
                                                                                      1. Anuani ya mwandishi
                                                                                                2. Tarehe
3. Mwanzo wa barua
                             4. Kiini cha barua
                                      5. Mwisho wa barua
                                                6. Jina la mwandishi


Mbinu za uandishi wa barua ya kirafiki.
[list=lower-roman]
[*]Matumizi ya lugha inayoeleweka
[*]Kutoa maelezo katika mtiririko mzuri
[*]Kuzingalia alama za uandishi, mfano; nukta(.)
[/list]
 

 
Mfano wa barua ya kirafiki
                                                   
                                                        Shule ya sekondari Arusha                                                            
                                                              S.L.P 5678
                                                                 Mkuranga
                                                                07/09/2017.
Kwako Mjomba                                                                                                            
Salama sana, ni matumaini yangu kuwa nyote hapo nyumbani ni wazima, mimi pia ni mzima.                                                                        Dhumuni la barua hii ni kutaka kukujulisha kuwa naendelea vizuri na masomo na mitihani yote tuliyofanya nimefanya vizuri lakini tunatarajia kufunga shule tarehe 30/07/2017, Wasalimu wote hapo nyumbani.                                                                                        
                       Mimi mpwa wako                                                                                                              
                        Rajabu Maridhawa                                                                                        


 
 
Hatua za kutuma barua
 1. Baada ya kumaliza kuandika barua ikunje na iweke kwenye bahasha
 2. Nenda posta na nunua stampu utaibandika juu ya bahasha upande wa kulia
 3. Tumbukiza barua yako katika kisanduku cha kupelekea barua
 
Uandishi Wa Anuani Juu Ya Bahasha
Juu ya bahasha huandikwa jina na anuani ya mpelekewa barua na nyuma ya bahasha huandikwa jina la mwandishi wa barua.