0
Application zimefunguliwa kwa ajili ya Yale Young African Scholars 2016. Mafunzo haya ya bure yanawaleta pamoja wanafunzi mbalimbali wa sekondari kutoka Africa kujifunza pamoja kwa siku 7, na kuwasaidia kujiandaa kwa ajili ya kuapply vyuo nchini Marekani. YYAS ni program rasmi ya Chuo Kikuu cha Yale University, kishirikiana na Higherlife Foundation.Maelezo ZaidiMafunzo ya 2016 yatafanyika katika maeneo matatu:
Ili kuapply, inabidi mwombaji awasilishe yafuatayo:
MyElimu itafurahi kumsaidia mwanafunzi yoyote katika kuapply kupata nafasi hii.
- Ghana: 29 July – 4 August
- Rwanda: 9 – 15 August
- Zimbabwe: 20 – 26 August
- Mwombaji inabidi awe bado ana mwaka mmoja uliobaki kumaliza masomo yake ya sekondari.
- Mwombaji inabidi awe na miaka kati ya 14 na 18 wakati wa program.
- Mwombaji inabidi awe raia wa nchi za Africa anayeishi ndani ya Africa.
- Waombaji watakaofanikiwa inabidi waonyeshe uwezo mkubwa kitaaluma, uwezo wa kiongozi, na kupenda yale yanayofundishwa kwenye program.
- Mwombaji inabidi aw tayari kufanya kazi na wenzake kama team.
- Waombaji wote watachujwa kwa usawa, na hakuna ufaulu wa chini unaotegemewa na hakuna mitihani utakayopewa ufanye. Hata hivyo inategemewa uwe na uwezo mkubwa kwenye kiingereza..
Ili kuapply, inabidi mwombaji awasilishe yafuatayo:
- Application form iliyokamilika – Fomu inapatikana hapa na inabidi ijazwe na na mwombaji.
- Barua moja kutoka kwa mwalimu – Barua hii itakuwa ni ya mwalimu akionyesha unafaa kushiriki kwenye program. Mwalimu anaweza kutuma barua hiyo kupitia link ataayotumiwa mwombaji kwenye email Njia nyingine, mwalimu anaweza kutuma barua hiyo kwa email kwenda african.scholars@yale.edu nayo itaambatanishwa kwenye file la mwombaji. Pia, waombaji inabidi wachague mwalimu ambaye yupo shuleni kwao anamjua mwombani vizuri na ameshamfundisha katika masomo yake.
- Matokeo rasmi ya mwombaji – Hii ni ripoti rasmi ya shule ikionyesha matokeo yako ya masomo ya darasani.
MyElimu itafurahi kumsaidia mwanafunzi yoyote katika kuapply kupata nafasi hii.