Lugha Kama Chombo Cha Mawasiliano
How to register and join MyElimu CLICK HERE

 
Thread Rating:
 • 0 Vote(s) - 0 Average
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4
 • 5
Lugha Kama Chombo Cha Mawasiliano
MyElimu Offline
System

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 121 in 79 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,952.25 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon  Lugha Kama Chombo Cha Mawasiliano

0
0
Maana ya Mawasiliano
Mawasiliano ni kitendo cha kubadilishana habari, taarifa au ujumbe baina ya watu wawili au zaidi kwa kutumia njia tofauti tofauti za mawasiliano mfano kwa njia ya maneno,njia ya simu au barua.
Mawasiliano anaweza kufanywa na watu ambao wapo karibu au sehemu tofauti tofauti.
DHANA YA LUGHA
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye kubeba maana ambazo zimekubaliwa na jamii fulani ili zitumike kwa lengo la kuwasiliana baina a jamii husika.
MUUNDO WA LUGHA
Kimuundo, lugha huundwa na vitu vinne:                   
1. SAUTI
Ni sehemu ndogo kabisa ya neno isiyoweza kugawanywa zaidi.
Mfano; “baki” kuna sauti nne yaani b,a,k, na i.
“kimbia” kuna sauti sita yaani k,i,m,b,i na a.
 
2. SILABI
Ni sehemu ya neno ambayo huundwa na sauti.                         
Mfano;”simama” lina silabi tatu yaani si,ma,ma,
* silabi  ‘si’  limeundwa kwa sauti mbili yaani  s  na  i.

3. MANENO
Ni muundo wa silabi moja au silabi kuanzia mbili na kuendelea ambazo zikiunganika kwa pamoja huleta maana.   
Mfano; “hayupo” ni neno linaloundwa na silabi tatu ambazo ni  ha,yu na po.

4. SENTENSI
Ni neno au maneno kuanzia moja na kuendelea yanayotoa ujumbe kamili.                                                
Mfano; “njoo” ni sentensi ya neno moja,
 “wataondoka kesho asubuhi” ni muunganiko wa maneno matatu .
Ni tungo ambayo hupatikana kutokana na muunganiko wa maneno matatu yaani wataondoka, kesho  na  asubuhi.

Mfumo huu wa lugha unaweza kuainishwa kwa ufupi namna hii;
Herufi + Herufi =   y + a = ya                                          Silabi + Silabi =  Neno  Kwa mfano;  ye + tu = yetu                                              Neno + Neno = Sentensi      Kwa mfano; yetu + haikufika =yetu haikufika

DHIMA YA LUGHA KATIKA MAWASILIANO
Lugha ni chombo ambacho huwawezesha wanadamu kupashana habari kwahiyo dhima kubwa ya lugha ni kupashana habari. Zaidi ya hapo lugha huwa na matumizi mbalimbali katika jamii. Yafuatayo ni Baadhi ya Matumizi yake:
Dhima za lugha katika jamii
1. Lugha ni utambulisho katika jamii - kwa kusikia watu wakiwa wanazungumza, tunapata kuwafahamu watu hao ni wa jamii gani au ni wa asili a wapi Kwa mfano; Mhehe akiwa anaongea kihehe tunapata kumtambua papo hapo kuwa mtu huyu ni mhehe
2. Lugha hutumika  kuwasilisha  hisia  - Kwa kutumia maneno lugha huweza kuonesha hisia mbalimbali kama vile upendo, wasiwasi, simanzi, watu wanapotambua hisia za wenzao hujua namna ya kushirikiana nao.
3. Lugha ni sehemu ya utamaduni wa watu, - vizazi na vizazi hurithishwa mila, desturi na tamaduni mbalimbali  za jamii kupitia lugha. Mfano kupitia nyimbo,hadithi,methali na maonyo mbalimbali.
4. Lugha hutumika katika shughuli za uzalishaji mali. - Huwaunganisha watu wanaofanya shughuli moja kwa hiyo lugha huleta na kuhimiza maendeleo.
5. Lugha huelimisha - watu hujifunza na kupata  maarifa stadi, mwelekeo wa maadili shuleni au popote pale kupitia lugha. 

LUGHA FASAHA NA UMUHIMU WAKE
Ufasaha ni utamkaji wa maneno katika lugha kwa usahihi ili kupata maana kamili na sahihi katika mazungumzo na maandishi.
Lugha fasaha ni lugha inayofata utaratibu na misingi ya lugha hiyo. Ufasaha unatokana na mpangilio wa maneno na miundo ya sentensi unaowasilisha maana a maneno yaliyotumika kwa usahihi.

Umuhimu wa kutumia lugha fasaha
 1. Hudumisha taratibu za kisarufi za lugha.
 2. Huhakikisha kukamilika kwa mawasiliano baina ya watu wanaowasiliana.
 3. Hudumisha lugha kwa kutegemea desturi za lugha hiyo
 4. Hutumika kukuza hadhi ya lugha.
 5. Huipa lugha urembo na mvuto unaofanya ipendeze inapotumika kwa ufasaha.
 
Madhara ya kutumia lugha isiyo fasaha
 1. Kuvunjwa kwa kanuni za sarufi.
 2. Kukwamisha mawasiliano.
 3. Kutozingatia kwa maadili.
 4. Kudumaishwa kwa lugha.
 
 
 
 
LAFUDHI
Ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira au lugha mama anayoituma siku zote.
Lafudhi inaweza kutambulisha jamii au eneo  analotoka mtu maana jinsi anavyotamka maneno huathiriwa zaidi na lugha mama aliyonao.
Mfano; Kupitia lafudhi tunaweza kutambua iwapo mtu ametoka kwenye jamii ya kihindi, kizungu.                                                                                                ;
Lafudhi hutambulisha mtu swarafia yake sababu ya athari za kimazingira.                   
Mfano “Msalimie sana shemeji yangu aisee (mchanga)”
 
UMBO
Umbo la neno hufuata tabia ya lugha yanayohusika, maneno ya Kiswahili hujengwa kwa sirabi kwa mfano kwa silabi zifuatazo  a-li-ku-nywa-da-wa hupatikana umbo la neno “alikunywa dawa”.
Muundo wa maneno ya Kiswahili huwa na silabi zenye irabu moja na konsonati moja au irabu moja au konsonati mbili au tatu na irabu moja
Kwa mfano chunguza tofauti kati ya maneno yafuatayo ya Kiswahili na yasiyo ya Kiswahili.
Mfano; Kiswahili                    sio kiswahli
           Kristo                           crystal
           Nyuni                            nyhen 
 
MPANGILIO
          Ni mpango wa  maneno kwa kutumia utaratibu maalum ili kuunda sentensi zinazotoa maana, Mpangilio wa maneno hutegemea aina ya maneno na kazi inayofanya neno katika sentensi husika .
Kusipofanyika mpangilio wa maneno kwa kutumia utaratibu maalum sentensi haiwezi kuleta maana.
Mfano;”Daktari mzuri amenipa dawa nzuri” au “Nzuri amenipa daktari dawa “
Mpangilio sahihi wa sentensi ungekuwa “Daktari amenipa  dawa nzuri”
 
MAANA
Ni dhana inayobebwa katika neno au sentensi ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa. Kila sentensi huwa na maana ambaondio inafanya mawasiliano yafanyike baina ya mtu mmoja au mwingine.
 
 

 

 
(This post was last modified: 10-20-2017, 12:19 PM by MyElimu.)
09-14-2017, 01:08 PM
Visit this user's website Find Like Post Reply


You may also like these discussions:
Thread Author Replies Views Last Post
  Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mablimbali MyElimu 0 7,047 12-04-2017, 02:24 PM
Last Post: MyElimu
  Umuhimu Wa Lugha Ya Kiswahili Sunday 0 5,775 09-21-2017, 12:32 PM
Last Post: Sunday
  Utumizi Wa Lugha MwlMaeda 2 8,605 06-20-2017, 12:58 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Tabia Na Sifa Za Lugha MwlMaeda 0 2,542 06-07-2017, 01:58 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mbalimbali. Damian 3 2,768 05-23-2017, 02:16 PM
Last Post: kemmyqlyon
Post Icon Nadharia Ya Ukuaji Na Ueneaji Wa Lugha MyElimu 0 7,969 02-07-2015, 05:09 AM
Last Post: MyElimuUsers browsing this thread: 2 Guest(s)