Maswali Ya Kiswahili 1 Form 5
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Maswali Ya Kiswahili 1 Form 5
MyElimu Offline
System
*******

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 119 in 79 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,945.20 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon Maswali Ya Kiswahili 1 Form 5

0
0
MAELEKEZO:
  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D
  2. Jibu maswali saba 7 kwa kuchagua swali (1) kutoka kila sehemu isipokuwa B jibu maswali (2).
  3. Zingatia mpango mzuri wa kazi na mwandiko unaosomeka.
  4. Fuata maelekezo na maagizo kwa kila swali.

 
SEHEMU A: UFAHAMU NA UFUPISHO
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yote.
 
(Nyumbani kwa mama Suzi: Wakati Mama Suzi anafua nguo anasikia mbisho wa hodi).
 
(kutoka nje) Hodi, hodi wenye nyumba!
 
MAMA SUZI :        Nyumba yako hii shoga  (Anainuka kuonana na mgeni. Anaingia mama Joti)
 
MAMA JOTI:         Vipi una safari?
MAMA SUZI:         Safari?
MAMA JOTI:         Ee naona unafua
MAMA SUZI:         (Huku anampa kiti) Shoga naye. Mtu hafai mpaka awe na safari? Umaridadi tu (wanacheka).
MAMA JOTI:         Haya mwenzangu za tangu jana?
MAMA SUZI:         Mh unadhani mimi nina cha kusema? Nina mfikiria Suzi wangu. Msiba wa Fausta umenitia woga.
MAMA JOTI:         Siyo wewe tu. Hebu niambie toto la mtu lile, lilivyokuwa limeenea vile. Si mashavu hayo, si macho, si ------ mh! mh! Mungu amuweke pema mtoto Fausta!
MAMA SUZI:         Mtoto kesha vile mpaka anageuka  kizuka! Nilitaka kukimbia ati, pale nilipotupa macho kwenye jeneza. Mtu si mtu, kizuka si kizuka!
MAMA JOTI:         Cha kushangaza ni pale tunapoambiwa eti kafa kwa kukanyaga  nyaya.
 
MAMA SUZI:         Kukanyaga nyaya? Mbona wengine wanasema kafa kwa  ukimwi?
MAMA JOTI:         Wewe nawe unakuwa nyuma nyuma kama koti? Mtu aliyekufa kwa kukanyaga  nyaya maana yake kafa kwa ukimwi.
 
MAMA SUZI:         Kiswahili cha siku hizi ni kigumu! (Anastuka) shoga unanisahaulisha kazi yangu. Anaendelea kufua) Lakini shoga watu wanatafuta maana ya marehemu. Kitoto kama kile; kife kwa ukimwi! Ungeingilia kona gani?
 
MAMA JOTI:         Wewe unamwona Fausta alikuwa mdogo? Ukubwa siku hizi siyo kuvunja ungo au ulikuwa unadanganywa na utakatifu wa usoni? Shoga, mtakatifu wa kwenye mwanga si lazima awe mtakatifu gizani.
 
MAMA SUZI:         Aa bwna mie siamini. Labda ungesema yalimkuta hayo kwa kuchangia wembe, kuchoma sindano isiyochemshwa au kuongezewa damu yenye virusi vya UKIMWI. Lakini jinsi ninavyoijua familia ile, Fausta asingeweza ama kufanya au kufanyiwa mambo haya. Kwanza Fausta alikuwa na afya njena sana katika uhai wake.
 
MAMA JOTI:         Chanzo cha kifo cha Fausta ni zinaa. (Kwa ukali kidogo). Shoga mbona unakuwa mgumu kama mpingo?
 
MAMA SUZI:         Fausta alikuwa mtoto sana mtoto wa darasa la tano mambo hayo asingeyajua.
 
MAMA JOTI:         Mwenzangu kwa nini tubishane? Haya…..
Taji vaa wewe umeshinda. (Anaingia Suzi akiwa amevalia sare ya shule)
 
SUZI:                    Shikamoo mama
MAMA SUZI:         Marahaba Suzi. Pole na shule
SUZI:                    Ahsante mama (Anaingia ndani)
MAMA SUZI:         Kile kitoto vile kilivyokuwa si kama hicho changu?
 
MASWALI
(a) Andika kichwa cha habari uliyoisoma
(b) Kwa mujibu wa mwandishi ukimwi unaambukizwaje?
© Kulingana na habari hii eleza mtazamo potofu uliojikita katika Jamii kuhusu maambukizi ya ukimwi.
(d) Mwandishi anazungumza nini kuhusu unyanyapaa?
(e) Unajifunza nini kupitia habari?
 
2.       Fupisha habari hii maneno yasiyozidi 30.
 
SEHEMU B: MATUMIZI YA SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
 
Jibu maswali mawili
 
3.       Eleza maana ya dhana zifuatazo
(a) Fonolojia
(b) Mofolojia
© Sintaksia
(d) Semantiksia
(e) Fonimu
 
4. Jadili mambo mbalimbali yanayodhoofisha lahaja.
 
5. Eleza kwa ufasaha hatua anazopitia mwanadamu kujifunza lugha ya kwanza.
 
6. Taja dhima za mofimu za maneno yafuatayo
    (a) Tumesomea
    (b) Hakiliki
 
SEHEMU C: UTUNGAJI
 
7. Andika Insha isiyozidi maneno 250 kuhusu ukimwi.
 
SEHEMU D: MAENDELEO YA KISWAHILI
 
8. Kwa kutumia ushahidi wa kiisimu thibitisha kuwa Kiswahili ni kibantu.
 
9. Fafanua hatua zilizochukuliwa na wakoloni wa kijerumani katika kukuza na kueneza Kiswahili nchini Tanzania.
 
SEHEMU E: FASIHI
 
10. (a) Nini tofauti ya Fasihi na sanaa
      (b) Usanaa wa fasihi unatokana na nini?
 

 
03-23-2015 09:27 AM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
utouh Offline
Regular User
Registered

Posts: 2
Likes Given: 0
Likes Received: 0 in 0 posts
Joined: Jul 2017
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 0.00 points
Post: #2
RE: Maswali Ya Kiswahili 1 Form 5

0
0
Naomba majibu swali la 9

Sent from my TECNO H6 using MyElimu mobile app
07-20-2017 08:34 PM
Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Elia Madete Offline
Regular User
Registered

Posts: 1
Likes Given: 2
Likes Received: 0 in 0 posts
Joined: Feb 2018
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 0.00 points
Post: #3
RE: Maswali Ya Kiswahili 1 Form 5

0
0
Naomba jibu swali la 8

Sent from my TECNO WX3 using MyElimu mobile app
02-18-2018 10:43 PM
Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
  Tofauti Ya Fasihi Ya Kiswahili Na Fasihi Katika Kiswahili Baynet 1 373 05-14-2018 02:38 PM
Last Post: Said Maganza
  Kiswahili For Beginners christine 0 312 03-14-2018 03:18 PM
Last Post: christine
  Umuhimu Wa Lugha Ya Kiswahili Sunday 0 4,900 09-21-2017 12:32 PM
Last Post: Sunday
  Kiswahili NAFTARI KAFUMU 0 818 09-14-2017 05:59 PM
Last Post: NAFTARI KAFUMU
Post Icon Methali Za Kiswahili MyElimu 26 510,347 09-07-2017 07:45 PM
Last Post: bensonrng
  Kiswahili john richard 0 573 08-12-2017 06:07 PM
Last Post: john richard
  Check Out "mwalimu Wa Kiswahili" MwlMaeda 0 1,409 07-27-2017 06:02 AM
Last Post: MwlMaeda
  Misemo,nahau Na Methali Za Kiswahili MwlMaeda 1 11,606 07-20-2017 08:24 PM
Last Post: utouh
  Jibu Maswali Yafuatayo MwlMaeda 0 871 06-21-2017 03:11 PM
Last Post: MwlMaeda
  Jipime Kwa Maswali Haya MwlMaeda 0 957 06-12-2017 11:01 PM
Last Post: MwlMaedaUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)