Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mablimbali
How to register and join MyElimu CLICK HERE

 
Thread Rating:
 • 0 Vote(s) - 0 Average
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4
 • 5
Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mablimbali
MyElimu Offline
System

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 120 in 79 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,951.25 points
Country: Tanzania
Post: #1
Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mablimbali

0
0
MATUMIZI YA LUGHA KATIKA MUKTADHA MBALIMBALI
Lugha ni sauti za nasibu zenye kubeba maana zinazokubalika katika jamii Fulani ili zitumike katika mawasiliano.
Utumizi wa Lugha
Ni namina ambayo wazungumzaji wa lugha Fulani wanazungumza kwa kuzingatia mila, destuli na tamaduni za jamii husika.
Dhima za Utumizi wa Lugha
 • Kupashana habari, ujuzi, maarifa,
 • Kuelimisha jamii
 • Husaidia kujenga uhusiano mwema baina ya watu, kwa mfano wafanyabiashara, wavuvi, wanafunzi na wafanyakazi mbalimbali
 • Husaidia kujua kutumia lugha kama inavyotakiwa
 • Husaidia kufikisha ujumbe kama ilivyokusudiwa
 • Husaidia kuepusha mgogoro katika jamii.
 
Msingi wa Matumizi ya Lugha
Mambo yanayoathiri matumizi ya lugha
 1. Mada inayozungumzwa, kwa mfano Mada inayohusu masomo, sherehe, msiba, au mazungumzo yanayohusu muziki lugha hutofautiana kutokana na mazingira hayo.
 2. Muktadha/ hii huhusisha mahali mazungumzo yanapofanyika, ni muhimu kuzingatia sehemu mazungumzo yanapofanyika, kwa mfano; mahakamani, jeshini, shuleni au kanisani.
 3. Malengo ya mazungumzo, malengo huweza kuwa ni ya kuelimisha, kukejeli au kutia moyo kwa hiyo.
 4. Uhusiano uliopo baina ya wazungumzaji, ni muhimu sana kuangalia uhusiano baina ya mtu unaezungumza nae, anaweza kuwa mwalimu, mzee, mwanafunzi mwenzako, au mzazi. Uhusiano baina ya watu huathiri pia matumizi ya lugha.
 5.  
Rejesta ni mtindo wa lugha ambayo maneno yake na mtindo wake wa kuongea huwa na dhumuni la kukidhi haja ya mawasiliano katika uwanja Fulani au mazingira maalumu.
Rejesta huonyesha anayezungumza yupo katika mazingira gani na hadhi yake ni ipi.
 
AINA ZA REJESTA
Aina za rejesta ziko nyingi kutokana na kukidhi haja ya mawasiliano katika uwanja Fulani wa mazungumzo;
[list=lower-roman]
[*]Rejesta za hospitalini

Aina hii ya rejesta hutumika hospitalini na mgonjwa akizungumza na daktari au mhudumu tofauti wa afya. Kwa mfano; “Ingia kwa daktari”, “chumba cha sindano”, “mgonjwa vipi hali yako”.
[list=lower-roman]
[*]Rejesta za hotelini

Hii hujumuisha maneno ambayo mara nyingi hutumika hotelini au kwa watu wengine ambao wanauza chakula, maneno haya yakitumika sehemu nyingine huweza kuleta tofauti katika maana zake, kwa mfano; “mimi nyama” nionyeshe menyu ya chakula”, “mimi chipsi kuku”
[list=lower-roman]
[*]Rejesta za dukani

Katika aina hii ya rejesta maneno ambayo hutumika ni yale ambayo hujumuisha mazungumzo kati ya mteja na muuza duka, kwa mfano; “mchele kilo moja”, mafuta ya kula robo”, “nipatie vocha”.
[list=lower-roman]
[*]Rejesta za kanisani

Hii hujumuisha maneno ambayo hutumika kwenye makanisani kati ya mchungaji na waumini wake au kati ya waumini na waumini, kwa mfano; Bwana asifiwe”, “ Sasa ni kipindi cha mahubiri”, “kwaya iimbe”.
[list=lower-roman]
[*]Rejesta za shuleni

Haya ni aina ya mazungumzo ambayo hutumika shuleni kati ya walimu na wanafunzi au wanafunzi pekee au walimu na walimu wenzao, kwa mfano; “Kusanyeni madaftari”, Ingieni darasani”, “wanafunzi achene kelele”.
 
Dhima za Rejesta
 • Husaidia kukidhi mawasiliano baina ya makundi mbalimbali, kwa mfano rejesta ya hotelini, rejesta ya mahakamani na jinsi zinazotumika tofauti kulingana na mazingira yake.
 • Hutambulisha wazungumzaji wa aina Fulani kutokana na aina ya rejesta wanayotumia.
 • Huficha ujumbe kwa watu wasiohusika na rejesta hiyo, mara nyingi rejesta huhusisha lugha ya mafumbo ambayo wahusika pekee huelewa.
 • Husaidia kufikisha ujumbe kwa njia fupi na ya haraka, kwa mfano; Rejesta ya hospitali, daktari akisema kutwa mara tatu, mgonjwa ni rahisi kuelewa nini kinachozungumzwa.
 • Husaidia kukuza lugha kutokana na kuongezeka misamiati mipya inayotokana na rejesta zinazozungumzwa.
 • Hupamba lugha, haswa kwa rejesta za mitaani.
 
MIISIMU
Ni lugha isiyo sanifu inayozungumzwa na kikundi Fulani cha watu wachache wenye utamaduni mmoja na baadae lugha hiyo hupotea, maneno yanayobaki husanifiwa na kuwa misamiati kamili ya Kiswahili.
Chanzo ya Miisimu
 • Mabadiliko yanayoikumba jamii, mabadiliko hayo yanaweza kuwa ya kisiasa, kiuchumi na kiikolojia, kwa mfano; Hari mpya, nguvu mpya na kasi mpya” yalizuka mwaka 2005.
 • Hali ya utani miongoni mwa watu mbalimbali, mara nyingi misimu hiyo inaweza kuwa kejeli, dharau au dhihaka.
Makundi ya Misimu
[list=lower-roman]
[*]Misimu ya kipekee

Aina hii ya misimu huwa haienei eneo kubwa , huzushwa na kikundi kidogo cha watu, kwa mfano wanafunzi, madereva, walimu au wavuvi.
 
[list=lower-roman]
[*]Misimu ya kitarafa

Aina hii ya misimu huenea eneo kubwa kidogo kimatumizi, huweza kuenea kwenye kata, tarafa, wilaya au mkoa, kwa mfano; Vifodi (vigari vidogo vya abiria Arusha).
[list=lower-roman]
[*]Misimu zagao

Aina hii ya misimu huenea eneo kubwa kidogo kimatumizi, huweza kufikia maneno kuzagaa katika nchi nzima, kwa mfano; maneno kama tapeli, bodaboda, au nyumba ndogo.
 
Dhima( Umuhimu) wa miisimu
 • Husaidia kuongeza misamiati, hii kutokea kwa misamiati inayodumu na kusanifiwa kuwa misamiati halali ya lugha.
 • Hutumika kupamba lugha, hii ni kwa ile miisimu ya kejeli, dhihaka na dharau, hufanya lugha ivutie kusikilizwa.
 • Hurahisisha mawasiliano na kufanya yaeleweke kwa haraka, mfano neno changudoa.
 • Huibua hisia mbalimbali, misimu kama vile fukara, hohehahe, wanyanyasaji na walalahoi.
 • Hutunza historia ya jamii husika, hutumika kukumbusha jamii kwa matukio ya kihistoria.
 
Sifa za Miisimu
 • Ni lugha isiyo sanifu
 • Huzuka na kutoweka
 • Ina chumvi nyingi
 • Ni lugha ya mafumbo
 • Hupendwa sana na watu
 
 
 
 
LUGHA YA MAZUNGUMZO NA YA MAANDISHI
Lugha ya Mazungumzo
Lugha ya Mazungumzo ni lugha ambayo hutolewa kwa njia ya mdomo, mazungumzo yanayotolewa yanakuwa na mzungumzaji na wasikilizaji.
Mzungumzaji na wasikilizaji wanaweza kuwa pamoja yaani ana kwa ana au wanaweza kuwa sehemu mbalimbali pia.
Lugha ya mazungumzo hutolewa kwa njia ya ;
[list=lower-roman]
[*]Mazingira ya ana kwa ana, kwa mfano mazungumzo ya nyumbani, darasani, mkutanoni, mahakamani au kanisani.
[*]Mazingira yasiyo ya ana kwa ana, kwa mfano; kupitia runinga, radio au kwa njia ya simu.

 
Faida za Lugha ya mazungumzo
 • Mzungumzaji anaweza kukaa ana kwa ana na wasikilizaji hivyo mazungumzo huimarisha mahusiano.
 • Mzungumzaji anaweza kupata nafasi ya kuuliza maswali kwa msikilizaji, pia msikilizaji anaweza kuuliza maswali.
 • Mzungumzaji anaweza kutumia ishara ya mwili katika kuwasilisha maelezo yake.
 • Mzungumzaji anaweza kuonyesha hisia zake kama vile kulia, kupaza sauti, kupunguza sauti au kuonyesha furaha au huzuni.
 • Mzungumzaji anaweza kupata nafasi ya kufuta usemi wake au kutoa maelezo ya ziada.
 • Mzungumzaji anaweza kubadilisha lugha yake kulingana na mazingira yaliyopo.
 • Mzungumzaji ana uhuru wa kutumia lugha ya mtaani kulingana na muktadha uliopo.
 
Matatizo ya Lugha ya mazungumzo
 • Kupoteza taarifa zilizotolewa, kwa sababu huhifadhiwa kichwani hivyo huweza kupotea kirahisi kama mtu atapoteza kumbukumbu
 • Ujumbe unaweza usieleweke vizuri unapotolewa kutokana na kelele nyingi
 • Mzungumzaji anayetumia lugha ya mazungumzo anaweza kurudia rudia maelezo bila sababu maalumu.
 
 
Lugha ya Maandishi
Hii ni lugha inayowasilishwa kwa njia ya maandishi, mazungumzo inawezekana yalifanyika kwa njia ya mdomo au kwa njia ya simu lakini yakawasilishwa kwa njia ya maandishi.
Lugha ya maandizi huzihusisha pande mbili ambazo ni mwandishi na msomaji, wakati mwingine mwandishi anaweza kuwa mbali na msomaji hivyo lugha inayotumika sharti iwe fasaha ili msomaji anaposoma maandishi apate kuelewa kila kitu kilichoandikwa na maana yake asiwe na maswali ya kujiuliza kutokana na kilichoulizwa.
Lugha ya maandishi hupaswa kuambatana na matumizi ya taratibu za uandishi ambazo ni pamoja na matumizi ya vituo, aya na herufi kubwa.
Ubora wa Lugha ya maandishi
 • Huwezesha watu walio mbali waweze kuwasiliana
 • Maelezo yanayoandikwa huwa ya kudumu kwasababu yakiwa yameandikwa hayawezi kufutika.
 • Hustawisha sarufi ya lugha na misingi yake hii ni kwa sababu mwandishi anahakikisha kwamba anazingatia kwa makini kanuni za kisarufi ili msomaji wake aweze kuelewa
 • Huwa na maelezo yanayoeleweka, hii ni kwa sababu mwandishi hulazimika kuandika kwa kuzingatia kanuni na miiko yote ya uandishi.
 
Udhaifu wa Lugha ya maandishi
 • Hutumika na wale tu wanaojua kusoma na kuandika.
 • Msomaji hukosa vidokezo vingi ambavyo katika mazungumzo ya ana kwa ana huchagia katika mawasiliano kuwa mazuri.
 • Humnyima mwandishi kupima uelewa wa wasomaji wake, kwa sababu mwandishi hawezi kuonana na msomaji wake.
 
Tofauti kati ya Lugha ya Maandishi na Lugha ya Mazungumzo#000000 solid;margin:15px;width:95%;">[td]
 1. Huwezesha mawasiliano kufanyika ana kwa ana
[/td][td]
 1. Mawasiliano hufanyika kwa njia ya maandishi
[/td][td]
 1. Haihitaji maandalizi kufanyika maana mzungumzaji huongea kile anachotaka kusema
[/td][td]
 1. Haihitaji sana kutumia kanuni za kisarufi
[/td][td]
 1. Mada katika mazungumzo huwa haziwi na uzito mkubwa
[/td][td]
 1. Viungo vya mwili huweza kutumika kuonyesha msistizo
[/td][td]
 1. Mpangilio wa muda na mawazo hautabiriki
[/td]
LUGHA YA MAZUNGUMZO LUGHA YA MAANDISHI
2.Huhitaji maandalizi,mwandishi sharti apate muda wa kuandika na kupitia vizuri kile alichokiandika
3.Huzingatia kanuni za kisarufi
4.Mada inayoelezewa huwa na uzito mkubwa
5.Wahusika hawaonani kwahyo hakuna matumizi ya viungo
6.Mpangilio wa muda na mawazo hutabirika na kunakuwa na mtiririko wa maelezo
 
Mambo ya Kuzingatia Katika utumiaji wa Lugha ya kimazungumzo na Lugha ya Kimaandishi
 • Mada inayozungumzwa, ili mazungumzo yaende vizuri wazungumzaji wanapaswa kuzingatia mada kwa mfano kama mada inahusu ndoa,mapenzi, unyago au kazi bila kuchanganya na vitu vingine.
 • Mazungumzo pia yanapaswa kuzingatia mazingira ambapo mazungumzo hayo yanafanyika, kwa mfano mazungumzo yatafanyika kijijini, mjini,shuleni au hotelini ili kuleta maana kutokana na mahali yanapofanyika.
 • Mazungumzo pia yanapaswa kuendana na malengo yaliyokusudiwa, ambayo inawezekana ikawa ni kuelimisha au kufafanua jambo Fulani ambalo halikueleweka vizuri.
 • Mahusiano yaliyopo kati ya wazungumzaji, Mazungumzo kati ya watoto wanaojifunza, wazee, viongozi au walimu hivyo mzungumzaji lazima azingatie uhusiano uliopo kati yake na anayezungumza nae.
 
MATAMSHI NA LAFUDHI YA KISWAHILI
Unapokuwa ukizungumza ni jambo muhimu kutumia lafudhi sahihi na kutamka maneno kwa usahihi kabisa. Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye kuzungumza lugha ya Kiswahili ni;
[list=lower-roman]
[*]Kutumia lugha sahihi
[*]Kutumia neno na maana yake kwa usahihi

 
Kutokuzingatia kanuni hizi kunaweza kusababisha kutokueleweka kwa maelezo yanayotolewa au habari inayozungumzwa.
Sababu za makosa ya matamshi na lafudhi
 1. Athari ya lugha mama
Ukiwasikia baadhi ya watumiaji wa lugha ya Kiswahili wanapokuwa wakizungumza unaweza kugundua haraka kuwa watumiaji hao wametoka kwenye jamii gani au wanatoka kwenye kabila gani.
Kwa mfano; Ondoa ukyafu(uchafu) hapa
Ukiangalia sentensi hiyo utabaini namna mzungumzaji alivyoathiriwa na lugha mama maana kwenye Kiswahili hakuna neno “ukyafu” bali uchafu.
 1. Dosari za ala za utamkaji
Baadhi ya watu hukosea kutamka neno kwa ufasaha kutokana na dosari katika ala za utamkaji. kuna ala mbalimbali za utamkaji wa maneno kwa mfano ulimi, mdomo, pua, koo na meno, hivyo ala mojawapo inapokuwa na dosari huathiri utamkaji wa maneno, kwa mfano thithi badala ya sisi kwa mtu mwenye upungufu wa meno
 
UTATA KATIKA MAWASILIANO
Utata ni hali ya neno au maneno katika sentensi kuwa na maana zaidi ya moja, kwa mfano;
[list=lower-roman]
[*]Nilikwenda na treni(Alikwenda na Treni) au (Aliongozana na treni)
[*]Nilileta mbuzi (mbuzi kama kibao cha kukunia nazi) au (Mbuzi mnyama anayefugwa)
[*]Barabara (Sawasawa) au (Njia ya kupita)

 
Chanzo cha Utata
 1. Neno lenyewe kuwa na maana zaidi ya moja.
Kwa mfano maneno kama barabara, mbuzi na kaa.
 
 1. Mtumiaji wa lugha kutokuzingatia taratibu za uandishi
Kwa mfano; Nilimkuta meshaki na rafiki yake Mwajuma
Maana1.Nilimkuta meshaki na rafiki wa mwajuma
Maana2. Mashaka na mwajuma ni marafiki, niliwakuta wote wawili
 
 1. Matumizi ya maneno ya lugha ya picha/taswira
Kwa mfano;Nina ua nyumbani kwangu
Maana1. Ua kama msichana mzuri
Maana2. Ua kama uzio wa kuzunguka nyumba
Maana3. Ua linalotokana na mti uliopandwa.
 
 1. Matumizi ya maneno pasipo kuzingatia muktadha au mazingira ya matumizi ya maneno.
 
 1. Kutamka maneno tofauti na inavyotakiwa
 
 
 1. Utumiaji wa viambishi katika vitenzi
Kwa mfano; Ana anampikia Juma ugali
Maana1. Ana anapika ugali kwa niaba ya Juma
Maana2. Ana anapika ugali ili Juma ale
 
         
 
 
 
 

 
12-04-2017, 02:24 PM
Visit this user's website Find Like Post Reply


You may also like these discussions:
Thread Author Replies Views Last Post
  Tofauti Ya Fasihi Ya Kiswahili Na Fasihi Katika Kiswahili Baynet 1 684 05-14-2018, 02:38 PM
Last Post: Said Maganza
  Umuhimu Wa Lugha Ya Kiswahili Sunday 0 5,438 09-21-2017, 12:32 PM
Last Post: Sunday
Post Icon Lugha Kama Chombo Cha Mawasiliano MyElimu 0 7,824 09-14-2017, 01:08 PM
Last Post: MyElimu
  Utumizi Wa Lugha MwlMaeda 2 7,780 06-20-2017, 12:58 PM
Last Post: MwlMaeda
  Kunani Katika Maisha Yangu Na Baada Ya Miaka Hamsini MwlMaeda 0 910 06-11-2017, 05:54 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Nyimbo Katika Fasihi Simulizi MwlMaeda 0 2,271 06-09-2017, 12:23 PM
Last Post: MwlMaeda
  Madoido Katika Fasihi MwlMaeda 0 943 06-07-2017, 10:57 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Tabia Na Sifa Za Lugha MwlMaeda 0 2,047 06-07-2017, 01:58 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Sifa Pambanuzi Za Kifani Za Utendi Andishi Wa Kiswahili Zinavyojitokeza Katika Utenzi MwlMaeda 2 2,614 06-07-2017, 01:38 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mbalimbali. Damian 3 2,545 05-23-2017, 02:16 PM
Last Post: kemmyqlyonUsers browsing this thread: 1 Guest(s)