Ufahamu
How to register and join MyElimu CLICK HERE

 
Thread Rating:
 • 0 Vote(s) - 0 Average
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4
 • 5
Ufahamu
MyElimu Offline
System

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 121 in 79 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,952.25 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon  Ufahamu

0
0
 
Maana ya ufahamu ni kuelewa jambo na kuweza kulifafanua baada ya kusikiliza, kusema au kuliona na kisha kulitafakari.   Ufahamu ni hali ya kulijua jambo na kuweza kulifafanua kwa ufasaha.
AINA ZA UFAHAMU
 1. Ufahamu wa kusikiliza
 2. Ufahamu wa kusoma
 3. Ufahamu wa kuona​​​​

1. UFAHAMU WA KUSIKILIZA
Ni aina ya ufahamu ambayo unasikiliza jambo linalosemwa na mtu mmoja kwa makini na utulivu kasha kuelewa na kulitafakari.

2. UFAHAMU WA KUSOMA
Ni ufahamu ambao unaweza kusoma jambo ambalo limeandikwa,msomaji aweze kusoma kwa sauti au kimya kulielewa na kasha kulitafakari jambo hilo.

3. UFAHAMU WA KUONA 
Ni ufahamu ambao mtu huona kitu/picha na kuweza kueleza ufahamu huu huibua hisia kwa mtazamaji.

DHIMA ZA UFAHAMU
Huokoa mda,ule ufahamu wa kuona na kusikiliza hakuhitaji kusoma kitabu utasikiliza tu na kuanza kulitafakari jambo.

Hupunguza gharama,hasa huelewa wa kusikiliza hauitaji fedha kwa ajili ya kununua kitabu ili kusoma.

Husaidia kutoa taarifa kwa ufupi na kwa usahihi,hii inatokana na kufuata maelekezo na maagizo utakayo yapata katika ufahamu wa kusoma

Ufahamu husaidia kukuza uelewa miongoni mwa wanafunzi,hii ni kwa sababu mwanafunzi anaposoma habari hutakiwa kubaini mawazo makuu na kasha kujibu maswali hivyo kiwango chake cha kuelewa hukua.

JINSI YA KUJIBU MASWALI YA UFAHAMU
Kichwa cha habari kuandikwa kwa herufi kubwa na kisizidi maneno matano.

Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma

Bainisha mawazo makuu

UFUPISHO
Ni kufupisha habari uliyosoma,uliyosikiliza au kuona kwa maneno machache bila kupoteza maana ya msingi ya habari.                                     Katika ufupisha unaweza ukatumia maneno yaleyale ama maneno yako mwenyewe lakini usipoteze maana ya habari hiyo.                                                         
Kwa kawaida maneno yanayobaki yanatakiwa yawe theluthi moja ya maneno ya awali.

DHIMA YA UFUPISHO
 1. Ufupisho unasaidia mambo makuu mawili:
 2. Kuokoa mda
 3. Kuokoa gharama
 
 
KUOKOA MDA
Hapa muda wa kuelezea jambo huwa mdogo hivyo kurahisisha mawasiliano kwani maneno huwa machache.
 
KUOKOA GHARAMA
Ufupisho husaidia kutumia nyenzo za uandishi chache hivyo hupunguza gharama.                                      
Mfano;
 1. Kaka wa mama yangu anaumwa ugongwa hatari wa ukimwi.
Ufupisho; mjomba anaumwa
 1. Amina ametumwa dukani kununua sabuni,kijiko,chumvi,beseni,sufuria
Ufupisho; amina ametumwa kununua vyombo vya ndani.

MBINU ZA KUFUPISHA
 • Tazama,soma au sikiliza habari kwa makini.
 • Rudia kusoma,kutazama au kusikiliza habari mara ya pili kubainisha mawazo makuu.
 • Andika habari kwa kifupi uliyoisomo,uliyoiona na kuisikiliza
 • Soma habari uliyoiandika kama haitofautiani maana na habari ya awali
 • Hakiki idadi ya maneno.

 
(This post was last modified: 10-20-2017, 01:21 PM by MyElimu.)
10-19-2017, 07:24 PM
Visit this user's website Find Like Post Reply


You may also like these discussions:
Thread Author Replies Views Last Post
  Ufahamu godhard 0 166 07-06-2018, 10:23 AM
Last Post: godhard
Post Icon Ufahamu Na Ufupisho (zoezi) MwlMaeda 0 1,620 06-07-2017, 02:16 PM
Last Post: MwlMaedaUsers browsing this thread: 1 Guest(s)